Uchumba wa Vanessa Mdee Njia Panda Baada ya Rotimi Kumpost EX Wake


Baada ya mchumba mpya wa staa wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee ‘V-Money’, Olurotimi Akinosho ‘Rotimi’ kuposti picha ya mwanamke ambaye inasemekana ni mchumba’ke wa zamani ‘eksi’, kwenye mitandao ya kijamii, uhusiano huo unadaiwa kuwa njia panda. Kurasa nyingi za udaku kwenye Mtandao wa Instagram, zimeishikia bango ishu hiyo huku zikidai kuwa penzi hilo linapumulia mashine au kuelekea kaburini. Lakini Gazeti la IJUMAA limemuweka Vanessa mtu kati na kutaka kujua mbivu na mbichi.

Vanessa amesema kuwa, watu waache kumsema kwa sababu Rotimi kumposti mpenzi wake wa zamani, haina maana kwamba wamerudiana au watarudiana.

“Kwani ni dhambi mtu kuposti picha ya mpenzi wake wa zamani? “Sioni tatizo kabisa kwani siyo kwamba eti wanataka kurudiana. “Unajua watu wanapenda kuongea, ninawashangaa sana. Wasifikiri mimi nitaachana naye (Rotimi), eti kwa sababu ya maneno yao.

“Sisi (Vanessa na Rotimi) tupo pamoja na watu wataendelea kutuona sana tu,” amesema Vanessa ambaye kabla ya kuwa na Rotimi ambaye ana asili ya nchini Nigeria, alikuwa kwenye uchumba na mwanamuziki Juma Mussa ‘Jux’ kwa miaka kadhaa kabla ya kutengana mwaka jana.

Hata hivyo, baadhi ya wadau wameendelea kumtahadharisha Vanessa juu ya mwanaume huyo kwani kuna madai ya kuwa Wanigeria hawadumu kwenye uhusiano na watu ambao siyo wa taifa lao.

Stori: NEEMA ADRIAN, Ijumaa


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad