Ujerumani Yatangaza Kufunga Mipaka yake Kuzuia Corona


Ujerumani imeamua kufunga mipaka yake na mataifa ya Austria, Uswisi na Ufaransa kuanzia kesho Jumatatu asubuhi katika hatua ya karibuni kabisa ya kupambana na kusambaa virusi vya Corona.

Hayo ni kulingana na magazeti mawili ya Der Spiegel na Bild yaliyoripoti kuwa mamlaka za Ujerumani lakini zitaendelea kuwaruhusu wasafiri wanaovuka mipaka kila siku kwa ajili ya kwenda kazini pamoja na uingizaji wa bidhaa.

Hata hivyo hakuna taarifa juu ya iwapo Ujerumani inalenga kuifunga pia mipaka mingine ikiwemo kati yake na Poland, Uholanzi, Denmark na Jamhuri ya Czech.

Hayo yanajiri wakati idadi jumla ya waliokufa kutokana na virusi vya corona duniani imepanda na kufikia watu 6,036. Ongezeko hilo ni kutokana na vifo vipya 105 nchini Uhisapania moja ya taifa lililoathiriwa vibaya na virusi vya corona barani Ulaya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad