UN: Corona itadhibitiwa kwa kutumia mantiki, si kwa kueneza taharuki



Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema dunia itafanikiwa katika vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Covid-19 (Corona) kwa kutumia mantiki, busara na tahadhari na wala sio kwa kueneza hofu na taharuki.

Antonio Guterres alisema hayo jana Jumapili na kuongeza kuwa, "huu ni wakati wa kutumia mantiki, wala si taharuki; wakati wa kutumia sayansi badala ya kunyanyapaa; na ni wakati wa kueneza kauli zenye ithibati na si porojo za kutia woga."

Guterres amesema ingawaje ni jambo la kibinadamu kupatwa na mshtuko na kuchanganyikiwa mwanadamu anapopatwa na 'tishio la kiafya' lakini utumiaji wa mantiki unapaswa kuzingatiwa na kupewa kipaumbele.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza bayana kuwa, licha ya Corona kutangazwa kuwa janga la kimataifa, lakini hatua za dharura zikichukuliwa kuanzia ngazi ya mtu binafsi, kitaifa na kimataifa basi dunia itafanikiwa kuudhibiti ugonjwa huo. 


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad