Usikatishwe Tamaa Kwa Kukataliwa Na Dunia

Kama upo kwenye mbio sahihi za mafanikio, kati ya kitu ambacho unatakiwa kujifunza sana ni kutokukatishwa tamaa na kukataliwa. Upo wakati utakataliwa kwenye biashara yako na kukosa wateja.

Hiyo haitoshi kuna wakati utakataliwa sana kwa kazi unayoomba na pia kuna wakati unaweza kukataliwa na mazingira na kushindwa kuvuna hata kile ulichopanda. Hiyo ni mifano michache kati ya mingi.

Kitu cha kujiuliza kukataliwa kwa namna yoyote kunapotokea kwako, huwa unachukuliaje? Huwa unajiona ni mpumbavu au mjinga au unakuwa unatumia kukataliwa huko kama sababu ya kusonga mbele?

Kwa wengi sina shaka sana kukataliwa kokote kunapotokea, ndani mwao hujisikia vibaya sana kiasi cha kwamba kutokutamani kuendelea tena. Je, hi ndiyo hali ambayo hutokea hata ndani mwako?

Usichokijua wapo watu wengi sana ambao walikataliwa mwanzoni na kazi zao lakini leo ni mabilionea. Sylvester Stalone alimaarufu Rambo alishindwa kupata uzamini wa kutoa filamu yake ya kwanza hadi aliuza mbwa wake.

Naye pia Alexander Graham Bell alipopeleka kwa mara ya kwanza kuiza teknolojia yake ya Simu  kwa Carl Orton ambaye ni mmliki wa Western union aliambiwa kampuni kubwa kama yake haiwezi kununua doli kama hilo.

Hebu jiulize ni kitu gani ambacho alikuwa akiwaza Rambo pale alipoambiwa hawezi kuigiza, au ni kitu gani alichokuwa akifikiri Bell pale alipoambiwa kazi yake ni hovyo na kufananishwa na doli?
Kwa ujasiri na ushujaa, hakuna aliyekata tamaa, waliamua kusonga mbele, leo hii dunia nzima inatumia simu na leo hii wengi wanamfahamu Rambo. Katika mazingira yoyote ulionayo hapo ulipo, usikubali kukatishwa tamaa na kukataliwa, simamia ndoto yako kikamilifu.

Ni kweli kuna wakati utapita katika mazingira magumu na kuonekama kila kitu kimekataa kabisa kwenye maisha, lakini hiyo usichukulie kwamba ndio uhalisia ulivyo. Chukua jukumu la kuendelea kusonga mbele.

Asikuzuie mtu kwa maneno yake, yasikuzuie mazingira yoyote yale, kitu cha msingi usikubali kushindwa kwenye akili yako kwanza, ukishindwa huko na huku nje utakuwa umeshindwa. Kabisa.
Hapo ulipo unajijua vizuri hali uliyonayo, hali hiyo kama huipendi sana amua kuibadili mara moja, kama unaona huoni matokeo ya haraka usikate tamaa, vumulia mambo yatakaa sawa kadri siku zinavyokwenda.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad