Virusi vya Corona: China yaripoti Hakuna Maambukizi Mapya ya ndani kwa Mara ya Kwanza
0
March 19, 2020
China leo imefikia hatua muhimu katika vita dhidi ya janga la virusi vya corona, baada ya kutangaza kutokuwepo na maambukizi mapya ya ndani kwa mara ya kwanza tangu kuzuka kwa mripuko, lakini maambukizi ya kutoka nje yanahatarisha maendeleo hayo.
Mji wa Wuhan ambao ulikuwa kitovu cha mripuko wa virusi vya corona mwezi Desemba, umeripoti kutokuwa na maambukizi mapya ya ndani, ikiwa ni mara ya kwanza tangu mamlaka zilipoanza kuchapisha takwimu mnamo mwezi Januari.
Mji huo ulio na wakaazi karibu milioni 11 uliwekwa chini ya karantini kuanzia Januari 23, huku wakaazi wengine milioni 40 katika jimbo la Hubei nao wakifungiwa siku zilizofuata.
Maisha yameanza kurejea kama kawaida katika maeneo mengine ya nchi, huku watu wakirejea kazini, viwanda kufunguliwa na shule zikijiandaa kuendelea na masomo katika baadhi ya mikoa.
Tags