Virusi vya Corona Vyawasotesha Njaa Machangudoa Ufaransa
0
March 26, 2020
Paris, Ufaransa. Huku afya zao zikiwa hatarini na wateja wakiyeyuka, machangudoa wanahangaika katika kipindi hiki ambacho virusi vya corona vinatishia maisha yao; hawaoni mwanga mbele.
Wengi wanalazimika kwenda mitaani katika wakati ambao polisi wanatekeleza amri ya serikali ya kuzuia watu kutoka nyumbani.
Ufaransa imekuwa katika amri ya kutotoka majumbani kwa wiki moja, huku safari muhimu tu za nje ndio zikiruhusiwa, ikiwa ni hatua za serikali kudhibiti kuenea kwa virusi vya corona.
"Sina njia, kuwa nafanya kazi mitaani, nasafiri kwenda katika makazi ya watu," alisema Pamela, msichana mwenye umri wa miaka 46 anayetokea kusini jiji lililo magharibi la Toulouse ambaye alisimama kufanya kazi hiyo wakati amri ilipotolewa.
Kupata fedha kwa njia ya kuuza miili kumepungua, alisema, lakini ameamua kupuuzia: "Lipa faini ya euro 147 ka mteja kwa mteja kwa kiwango cha euro 50, hapana…"
Hata hivyo, kama amri hiyo itaendelea, akiba yake ndogo haitatosha, alisema.
"Nitalazimika kujitoa muhanga. Hata kama nina wateja wawili kwa wiki, (fedha nitakayopata) itatumika angalau kulipia chakula," alisema.
Jina lake na ya wengine waliozungumza katika habari hii, yamebadilishwa.
"Hali ni ya aina yake," anasema Sarah-Marie Maffesoli, mratibu wa programu wa taasisi ya madaktari wa haki za binadamu duniani.
"Ni kama hakuna tena wateja. Watawezaje kuacha kufanya kazi?" alisema.
"Kuwa na afya njema bila ya kuwa na uwezo wa kula au kumlisha mtoto ni kitu kigumu."
Uchangudoa hauruhusiwi kisheria Ufaransa, ingawa sheria iliyopitishwa mwaka 2016 inahalalisha kununua ngono, hivyo kuhamishia mzigo wa kosa kwa wateja ambao wanaweza kulipishwa faini wakikamatwa.
Lakini wanaouza miili, wachache wao wakiwa na hadhi ya kujiajiri, hawataweza kudai euro 1,500 (zaidi ya Sh3 milioni) za msaada ulioahidiwa na serikali kwa wafanyakazi walioajiajiri kufidia kupungua kwa kazi zao kunakotokana na mlipuko wa virusi vya corona
Tags