Vyombo vitatu vya habari vyapigwa faini ya sh.milioni 11




MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania(TCRA) kupitia Kamati ya

Maudhui mtandaoni, imevitoza faini ya sh.milioni 11 vyombo vya habari vitatu kwa kukiuka kanuni za mawasiliano ya kielektoniki na posta.

Vyombo hivyo ni Radio Classic FM, Luninga mtandaoni ya Sami Misago na Rock Media Group.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui, Joseph Mapunda amesema lengo la kamati kufanya hivyo ni kuimarisha tasnia ya habari nchini kwani inatakiwa kuwa na ubunifu usiovuka mipaka kutokana sheria za leseni walizopewa.

"Suala la utangazaji linahitaji watangazaji wabunifu na walio na elimu ili kutumia lugha zisizoleta athari kwa jamii, hivyo nashauri uongozi kuweka usimamizi mzuri kwa wafanyakazi wao ikiwa kuwaongezea kiwango cha elimu na kutambua miiko ya waandishi katika utoaji wa taarifa ,"amesema Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maudhui

Mapunda amesema Redio Classic kupitia kipindi cha Pepeta waliwadhalilisha waislamu kwa kutumia lugha ya kiarabu na kukiuka kanuni za mawasiliano ya kielektoniki na posta kutokana na masuala ya imani yanatofautiana uvumilivu.

Amesema baada ya kutokea hivyo kamati iliwaita wahusika kwa ajili ya kuwahoji na wao kuweza kutoa utetezi kwa nini wasichukuliwe hatua za kisheria ambapo waliahidi kusimamia misingi ya utangazaji na kutaka kuomba radhi siku saba kuanzia Machi 18.

Makamu mwenyekiti huyo alisema tathmini ya kamati baada ya kuwahoji ilibaini redio hiyo imefanya kosa la kutokuwa waangalifu kwa kutangaza maneno yenye ukakasi kwa jamii.

Kamati hiyo iliamua kuwatoza faini ya sh. 1,000,000 na kuwapa onyo kali na haki ya kukata rufaa kwenye Baraza la Haki ya Kibiashara iko wazi ndani ya siku 21 kuanzia sasa.

Kwa upande mwingine TCRA imewatoza faini ya sh.milioni tano luninga mtandaoni ya Sami Sago kwa kuchapisha maudhui ya matusi.Sami Sago nao wamepewa onyo kali kwa kutakiwa kutorudia tena na kuwaomba radhi watazamaji wao kwa siku saba mfululizo na rufaa ipo wazi ndani ya siku 21 kutokana na kuchapisha picha ya mwanamke kunyanyua kiuno juu na kufanya kushabikia vitendo.

Kamati hiyo ya maudhui ya TCRA imetoza faini ya sh.milioni tano luninga mtandaoni ya Rock Media Group, kwa kutangaza taarifa bila ulinganifu na kuwadhalilisha wananchi wa Bagamoyo.

Hata hivyo wametakiwa kuomba radhi ndani ya siku saba mfululizo na kupewa onyo kali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad