Wabunge watatu wa Chadema wamelazwa hospitali


Dar es Salaam. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kinaendelea kufuatilia hali za wabunge watatu waliolazwa hospitali baada ya kudai kupigwa na polisi.
Viongozi wanne wa chama hicho na wanachama zaidi ya 16 jana  walikamatwa na polisi wakati wakifuatilia kuachiwa huru kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ambaye alikuwa katika gereza la Segerea.

Akiongea na Mwananchi leo Jumamosi Machi 14, 2020 Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema viongozi hao baada ya kupata dhamana walipelekwa hospitali ya Aga Khan.
"Tumetuma viongozi wetu wanafuatilia kwa sasa bado asubuhi baada yakupata taarifa ya hali zao tutawafahamisha," amesema Mrema.
Amesema Mbunge wa Kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda, Ester Bulaya wamelazwa katika hospitali ya Aga Khan na Mbunge wa Viti Maalum, Jesca Kishoa alilazwa hospitali ya Amana.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad