Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema idadi ya wagonjwa wa corona imefikia 13 ambapo kati yao 8 ni Watanzania na watano ni wageni
Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Machi 26, 2020, wakati akitoa taarifa kwa umma, kuhusu hali ya maambukizi ya virusi vya Corona nchini
Amesema kati ya wagonjwa hao Dar es Salaam wapo nane, Arusha wawili, Zanzibar wawili na Kagera mmoja.
Waziri Ummy amesema kuwa mgonjwa wa 13 alipatikana mkoani Kagera na ni dereva wa magari makubwa, ambaye aliingia nchini kupitia mpaka wa Kabanga na shughuli zake anafanyia kati ya Burundi, DRC na Tanzania.
Pia amesema mgonjwa wa kwanza nchini wa virusi vya corona, Isabela Mwampamba (46) ameshapona ugonjwa huo.
“Mgonjwa wetu wa kwanza ambaye haturuhusiwi kutaja jina lakini alijitaja mwenyewe amepona COVID 19, tumepima sampuli mara tatu na zote zimeonyesha negative, tumeanza utaratibu wa kumruhusu kurudi nyumbani,” amesema.