Watu wawili waliopatikana na virusi vya Corona ni wale waliotangamana na mgonjwa wa kwanza.
Akizungumza na umma wa Wakenya moja kwa moja kupitia televisheni rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta amesema masomo katika shule taasisi zote yamesimamishwa mara moja.
Shule za msingi na sekondari zitafungwa kuanzia Jumatatu huku bweni zitafungwa ifikapo Jumatano amesema rais Kenytatta.
Vyuo vikuu na vyuo pamoja na taasisi nyingine za elimu zitafungwa ifikapo Ijumaa na pale inapowezekana waajiriwa wanapaswa kuruhusiwa kuhfanya kazi nyumani kwao ili kuepukana na maambukizi ya coronavirus.