Botswana, ni moja kati ya nchi za kidemokrasia zinazoendeleza adhabu ya kifo. Machi 28, 2020, Moabi Seabelo Mabiletsa (33) na Matshidiso Tshid Boikanyo (39) walinyongwa hadi kufa katika mji mkuu wa Botswana, Gaborone
Wawili hao walimuua dereva wa taksi miaka sita iliyopita. Kabla ya hawa kuna mwingine alinyongwa mwezi Februari na mwingine mwezi Desemba mwaka jana. Hii ndio nchi pekee kusini mwa Afrika inayotekeleza adhabu ya kunyongwa
Hii inafanya jumla ya watu wanne kuwa wamenyongwa tangu rais Mokgweetsi Masisi achaguliwe kuingia madarakani Aprili 1, 2018. Adhabu ya kifo ipo kisheria tangu walipopata uhuru wao toka kwa Uingereza mwaka 1966
Kwa mujibu wa Amnesty International, nchi 195 duniani zimefuta adhabu ya kifo au wameacha kuzitekeleza kwa zaidi ya miaka kumi iliyopita