Wanyama wavishwa ‘Maski’ kukingwa na Virusi vya Corona



Wakati duniani ikiendelea kutafuta suluhisho la kutokomeza Virusi vya Corona, baadhi ya watu nchini China wamebuni njia za kuwalinda wanyama wao dhidi ya ugonjwa huo.



Picha hii inayomuonyesha paka akiwa amevalishwa maski usoni ili kuepukana na Virusi vya Corona imewavutia watu wengi na kusambaa kwenye mitandao ya kijamii nchini China, hali inayoonyesha ni kwa kiasi gani mmiliki wa mnyama huyo alivyokuwa na mapenzi pamoja na kumjali mnyama huyo.



Licha ya kuwa picha hiyo aionyesha wazi eneo la China ambalo ndipo ilipopigwa lakini kwa mujibu wa Ten Cent News inadai kuwa baadhi ya watu wengi wanaomiliki wanyama sasa wamelibeba wazo hilo na kulifanyia kazi.

epa08234160 A woman wearing a face mask holds her dog, also wearing a face mask, in Guangzhou, Guangdong, China, 21 February 2020. The disease COVIDF-19, caused by coronavirus SARS-CoV-2, has so far killed 2,247 people with over 76,200 infected worldwide. EPA/ALEX PLAVEVSKI

Hata hivyo kwa mujibu wa World Health Organisation (WHO) hakuna ushahidi kuwa wanyama wanaweza kuathirika na ugonjwa huo wa Virusi vya Corona.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad