“Harufu inaweza ikatoka mdomoni au ikatoka sehemu nyingine ambazo sio mdomoni, stress pia zinasababisha mdomo kutoa harufu, unapokuwa na stress unaathiri mtiririko wa damu na mate, na mate yanasaidia kusafisha meno na mdomo kwahiyo yasipokuwepo ya kutosha Bacteria mdomoni wanashindwa kusafishwa" - Dkt.Ambege Mwakatobe, Rais wa Chama cha Wataalamu wa Afya ( ya kinywa na meno)
Dkt.Mwakatobe amesema mwaka huu siku ya afya ya kinywa na meno Kitaifa itafanyika Katavi na wanatarajia kuwahudumia Watu zaidi ya Elfu 90 katika Mkoa huo kwa kuwatibu matatizo ya kinywa na kutoa ushauri.