Watu 291 walioathirika na virusi vya Corona wamepona Iran


Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Udaktari nchini Iran imetangaza kwamba hadi sasa watu 291 waliokuwa wameathirika na virusi vya Corona wamepona na kuruhusiwa kutoka hospitalini.

Alireza Raeesi, Naibu Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Udaktari nchini Iran ameyasema hayo leo akiongea na waandishi wa habari. Ameashiria kuwa watu 1,501 waathiriwa wa virusi vya Corona nchini Iran na kusema kwa bahati mbaya hadi sasa watu 66 wamefariki dunia kutokana na virusi hivyo.

Virusi vya Corona viliibuka kwa mara ya kwanza katika mji wa Wuhan nchini China. Kidhahiri virusi hivyo vinatokana na wanyama wasio wa kufugwa. Virusi hivyo vimeenea katika nchi nyingine 70 za dunia.Alireza Raeesi, Naibu Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Udakktari nchini Iran

Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni, hadi sasa zaidi ya watu elfu 89 ameathirika na virusi vya Corona kote duniani ambapo kati yao watu elfu 45 wamepona huku wengine zaidi ya 3000 wakifariki dunia.

Kwa sasa wimbi la kuenea virusi vya Corona duniani limezusha wasiwasi mkubwa na jamii ya madaktari nchini Iran iko mstari wa mbele kwa kufanya kazi usiku na mchana katika kupambana na virusi hivyo vinavyoenea kwa kasi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad