Watu 913 wapona virusi vya corona nchini Iran, WHO yapongeza



Wizara ya Afya ya Iran imetangaza kuwa hadi hivi sasa watu 913 walioambukizwa virusi vya corona humu nchini wamepona na kurejea katika maisha yao ya kawaida.

Dk Kianoush Jahanpour, Mkuu wa Kituo cha Mawasiliano ya Umma na Upashaji Habari cha Wizara ya Afya ya Iran alitangaza habari hiyo jana Ijumaa na kuongeza kuwa, watu walioambukizwa virusi vya corona nchini Iran kufikia jana ilikuwa ni 4,747, kati ya hao 124 wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo lakini waliopona ni watu 913.

Dk Jahanpour aidha amesema, zaidi ya kesi 15,981 za watu walioshukiwa kuwa na virusi vya corona zimechukuliwa vipimo na kufanyiwa majaribio humu nchini ambapo kati ya kesi hizo zote, ni 4,747 ndizo zilizothibitika ni za virusi vya corona.

Wimbi la maambukizi ya virusi vya corona lilianza mwezi Disemba 2019 mjini Wuhan China na inavyoonekana ni kwamba wanyama wa kufuga majumbani ndio chanzo cha kuenea virusi hivyo.
 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad