Watu Wanne wa Familia Moja Wamefariki kwa Kuvuta HEWA ya ukaa Yenye Sumu Wakiwa Wamelala


WATU wanne wa familia moja katika kitongoji cha Ngilimba B kijiji cha Ngilimba kata ya Ulowa Halmashauri ya Ushetu Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga, wamepoteza maisha baada ya kuvuta hewa ukaa yenye sumu (Carbon monoxide) usiku wakiwa wamelala.

Kamanada wa jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga ACP, Debora Magiligimba alisema tukio hilo lilitokea machi 28, 2020 majira ya saa tisa usiku katika kitongoji na kijiji cha Ngilimba kata ya ulowa Wilaya ya kipolisi Ushetu.

Alisema chanzo cha tukio hilo ni mvua kubwa iliyonyesha kijijini hapo na kusababisha kuwepo kwa baridi nyumbani kwa marehemu,ndipo wakati wakijiandaa kulala waliwasha ndani jiko la mkaa likiwa linawaka.

Kamanda alisema walifunga milango yote na madirisha hali iliyosababisha kuwepo kwa hewa ndogo ndani ya nyumba yao na kuvuta hewa hiyo iliyokuwa na sumu ya Carbon monoxide.

“Mvua ilinyesha kubwa huko ulowa na kusababisha kuwepo kwa baridi,waliwasha jiko la mkaa na wakati wanajiandaa kwenda kulala,walifunga madirisha na milango na kusababisha kuwepo kwa hewa chafu yenye sumu ambayo imesababisha kupoteza maisha yao”Alisema Magiligimba.

Aliwataja kwa majina kuwa ni Masanja Emmanuel(35) msukuma na mkulima, Mngole Masanja (25)Mhangaza mkulima mkazi wa Ngilimba, Holo Masanja (5) Msukuma, Matama Masanja ambae umri wake haukufahamika kwa haraka wote wa familia moja.

Alisema kuwa,Miili ya marehemu imekabidhiwa kwa ndugu kwaajili ya mazishi baada ya kufanyiwa uchunguzi wa daktari na kuwataka wananchi kuacha kufunga milango na madirisha endapo watalala ndani huku wakiwa wamewasha jiko la mkaa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad