Watu wanne wajitolea kufanyiwa chanjo ya corona


Washington, Marekani. Watu wanne wanafanyiwa jaribio ya chanjo ya kinga dhidi ya virusi vya corona nchini Marekani.

Utafiti huo unafantwa na kampuni ya teknolojia ya masuala ya vimelea vya magonjwa ya Moderna Therapeutics.

Shirika la habari la Associated Press lilisema kuwa watu hao walichomwa sindano ya virusi vya corona katika kituo cha utafiti cha Kaiser Permanente kilichopo katika mji wa Seattle, Washington.

Kwa mujibu wa shirika hilo, chanjo hiyo haiwezi kusababisha covid-19 lakini ina jeni la virusi ambavyo vinaweza kusababisha ugonjwa huo.

Hata hivyo, wataalamu wa afya nchini humo walisema itachukua miezi kadhaa kujua ikiwa chanjo hiyo utafanikiwa.

Shirika hilo lilisema kuwa mtu wa kwanza kujitolea kuwekewa dozi ya kwanza ya utafiti huo ni mama wa watoto wawili mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Seattle, Washington.


"Hii ni fursa ya kufurahisha kwangu kuweza kufanya kitu fulani," alisema mama huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jennifer Haller

Shirika la habari la AFP lilisema kuwa hilo ni jaribio la kwanza kwa binadamu, lililodhaminiwa na Taasisi ya Kitaifa ya Afya nchini Marekani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad