Waziri Kigwangalla APEWA za uso Mtandaoni Baada ya Kauli yake Kwa Wapinzani Kuwatoa Wenzao Jela



Waziri wa Maliasili na Utali, Dk. Hamis Kigwangalla, ameshambuliwa vikali katika mtandao wa kijamii kuhusiana na kauli yake aliyoitoa ya kufanya siasa kwenye mambo ya kisheria

Kigwangalla aliandika ujumbe huu katika ukurasa wake wa twitter
“Mmefanya siasa kwenye mambo ya kisheria na haki! hongereni kwa kuwatoa though,”

Awali mjumbe mmoja katika ukurasa huo aliandika hivi
“Mhe. unafahamu kwamba tumefanikiwa kuwaondoa matatizoni wabunge wetu. huu ndio ushahidi wa upendo wa Watanzania kama walivyosaidia Frelimo na ZANU-PF kujikomboa na ukandamizaji wa kikoloni.

Baada ya Kigwangalla kumjibu baadhi ya mashabiki wa twitter katika ukurasa huo walimtukana matusi huku wengine wakihoji mbona chama chake kupitia polepole wamemlipia mwanachama wao Vicent Mashinji
“Si bora sisi tunamini viongozi wetu hawana hatia kulikoni nyinyi mliomtoa mtu mlie sema amesababisha kifo cha Akwilina.

Baaada ya kuona anashambuliwa Kigwangalla alijibu hivi “Hawana hatia? sasa kama hawana hatia mbona wametumikia adhabu? si wangekata rufaa,” alihoji Kigwangalla.

Mwingine aliandika ujumbe huu “Kwa hiyo nia ilikua wateseke jela? mbona hii tweet ni ya kejeli sana,” aliandika Tayanah

“Mheshimiwa nataka kukuhakikishia kuwa wana CCM hawawezi kamwe kufanya hiki wanachokifanya Wapinzani. nyie mtapata michango ya wafanyabiashara wakubwa na makampuni ambayo yanaogopa kuadhibiwa kama wasipochangia,”aliandika Innocent M.W

Wakili wa kujitegemea alihoji “Kwani kesi yao ilikuwa si ya kisiasa? si mlisema watolewe bungeni ili muwafix mitaani? lakini asanteni kwa kuwa wananchi hongera maana ndiye weenye nchi,”

Mentor Jofrey
“Ulitakaje Hamis? kwamba hiyo sheria ndo ilifanya hukumu ya kuwakomoa? #think twice.. ndio wakati mwingine huwa naku-critisize sana kwa mambo yako ya hovyo na maneno yako ya dharau na kejeli jitahidi kubalance shobo bro,”

“Bora ungekaa kimya unazidi kunichefua …sijui unaakili za namna gani we kijana,” aliandika David Mwakatumbula.
Kigwangalla alijibu kuwa
“Akili zangu za kifalsafa. kwa hiyo mtu mwepesi hivi hawezi kunielewa hata siku moja,”.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad