Zitto Aanza Mchakato wa Kuchangisha Fedha Kupunguza Mzigo wa Hukumu kwa Viongozi wa Chadema



Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe ameanzisha utaratibu wa kuwachangia fedha viongozi wa Chadema muda mfupi baada ya kuhukumiwa kulipa mamilioni ya Shilingi.

Viongozi wa chadema akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho Vicent Mashinji wamehukumiwa leo kulipa zaidi ya Sh300 milioni.

Baada ya hukumu hiyo Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma mjini amesema faini hiyo ni kubwa hivyo haiwezi kuachwa ikawa ni mzigo wa wanachadema pekee.

“Kila mtanzania mpenzi wa demokrasia nakushawishi tuanze mchango wa kuwachangia fedha wenzetu wa Chadema”.

Baada ya wachangiaji katika mtandao wa Twitter wametaka kuelekezwa namna ya kuwasilisha michango lakini kuna waliosema michango hiyo isimuhusu Mashinji ambaye hivi sasa amehamia CCM.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad