Zitto Kabwe Aishauri Serikali Namna ya Kuokoa Uchumi Kipindi Hichi cha Corona Virus
1
March 18, 2020
Serikali imethibitisha uwepo wa #CoronaVirus nchini. Zitto Kabwe ameshauri Serikali haya ili kuhami uchumi nchini
Amesema watu wetu ni fukara sana, bei za chakula zitapanda na wengi hawatamudu. Pia Serikali ina nafaka ya kutosha Siku 3 tu kwa kila Mtanzania. Ni vema Serikali kufanya uamuzi wa haraka kununua chakula ili kukigawa maeneo itakapohitajika
Ameongeza kuwa Serikali itazame namna ya kuwafidia ‘stimulus package’ wafanyabiashara katika sekta hiyo ili kulinda ajira za Wananchi. Ikiwezekana fidia iwe ni kulinda ajira kwa kufidia gharama za wafanyakazi ‘payroll costs’
Amemshauri Waziri wa Fedha kupeleke Bungeni Taarifa ya utafiti wa madhara ya mlipuko wa Corona kwa Uchumi wa Tanzania kwa ujumla na Bunge lijadili Kwa maslahi ya Taifa ili kutoa mapendekezo ya kibajeti kuhami Uchumi wa Nchi yetu na haswa kulinda biashara ndogo, Wafanyakazi kwenye sekta zilizo hatarini
Tags
Wewe fatilia kesi zako.
ReplyDeleteNchi inao wachumi wanaotambulika na Si fake na Kilaza kama wewe.
Kisutu wanakungoja kwa SIMBA. Mchochezi usiye itakia meme nchi ulio zamia. Nimeona w engine wakitolewa Goma mpaka Bukavu Jana. Shauri yako Dogo...!!!