Zitto Kabwe na Kesi yake ya Uchochezi Kuanza Kujitetea


Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe, leo Machi 17, 2020 ataanza rasmi kujitetea kwa siku nne mfululizo hadi Machi 20, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es Salaam, kufuatia kesi yake ya uchochezi inayomkabili.



Februari 18, 2020, Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu chini ya Hakimu mwandamizi Huruma Shaidi, ilimkuta kiongozi huyo na kesi ya kujibu, ambapo pia jumla ya mashahidi 10 wanatarajiwa  kumtetea.

Zitto anakabiliwa na mashtaka matatu ya uchochezi, anayodaiwa kuyatenda Oktoba 28, 2018 katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya chama hicho Kijitonyama Dar es Salaam.

Mashtaka ya Zitto yanatokana na kauli zake za kulitaka jeshi la Polisi, kutolea maelezo kwa kile alichokiita mauaji ya Polisi na raia, yaliyotokea kwenye Kijiji cha Mpeta, Wilayani Uvinza, Mkoani Kigoma.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad