Mfahamu Mwanamke Aliyegundua VIRUSI vya Corona Kabla ya Covid-19...Aliacha Shule Akiwa na Miaka 16


Mfahamu Mwanamke Aliyegundua VIRUSI vya Corona Kabla ya Covid-19...Aliacha Shule Akiwa na Miaka 16
Mwanamke aliyegundua kwa mara ya kwanza virusi vya corona kwenye mwili wa binadamu, alikuwa binti wa dereva wa basi aliyeacha shule akiwa na miaka 16.

June Almeida alijiendeleza na kuwa kinara wa kugundua picha za virusi, na kazi yake imekumbukwa wakati huu wa mlipuko wa corona.

Ugonjwa wa Covid-19 ni mpya lakini virusi vya corona si vipya , viligunduliwa kwa mara ya kwanza na Dkt Almeida mnamo mwaka 1964 katika maabara ya hospitali ya St Thomas' mjini London.

Mtaalamu huyo wa virusi alizaliwa mwezi Juni mwaka 1930 na kukulia kaskazini mashariki mwa Glasgow, nchini Scotland.

Aliacha kusoma shule ya kawaida akiwa mdogo na kupata ajira katika maabara.

Baadae akaamia London kujiendeleza taaluma yake na mwaka 1954 aliolewa na Enriques Almeida, ambaye alikuwa ni msanii raia wa Venezuela.

Utafiti wa mafua ya kawaida
Wanandoa hao pamoja na binti yao walihamia Toronto nchini Canada na kwa mujibu wa muandishi wa masuala ya afya George Winter, Dkt. Almeida aliendeleza ujuzi wake wa kugundua vijidudu kwa darubini ya umeme katika taasisi ya kansa ya Ontario.

Alikuwa mairi katika ujuzi wa kubaini vizuri virusi mbalimbali.

Bwana Winter aliiambia BBC kuwa kipaji cha mwanamke huyo kiligunduliwa nchini Uingereza mwaka 1964 alipoanza kufanya kazi taasisi ya afya ya St Thomas mjini London, hospitali ambayo ilimtibu waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson wakati alipougua ugonjwa wa Covid-19.

Aliporejea shuleni hapo kama mfanyakazi alikuwa akishirikiana na Dkt David Tyrrell, ambaye alikuwa anafanya utafiti kuhusu mafua ya kawaida.

Bwana Winter alisema Dr Tyrrell aikuwa akifanyia utafiti baadhi ya vijidudu ambavyo vinasababisha mafua .

Sampuli moja , ambayo ilikuja kugundulika kama B814,ilikuwa imetoka kwenye sehemu ya kunawia ya shule ya bweni huko Surrey mwaka 1960.

Waliweza kubaini kuwa virusi hivyo vina dalili za vijidudu vya mafua ya kawaida lakini waliweza kuona kuwa vijidudu vyake viko tofauti na vingine.

Ingawa , utafiti huo waliofanya pamoja na vijana wa kujitolea pamoja na Dkt Tyrrell aliona bora vijijidudu hao waangaliwe kwa darubini ya umeme.

Hivyo wakaamua kutuma sampuli kwa June Almeida ambaye aliweza kuona virusi hivyo kuwa vinaambukiza mafua lakini zinaonekana kuwa hazifanani sana.

Na virusi hivyo vilikuja kubainika kuwa ndio mara ya kwanza kubainika katika mwili wa binadamu.

Uchunguzi huo ulikataliwa
Bwana Winter anasema kuwa kile ambacho kiligunduliwa na Dr. Almeida vilikuwa vijidudu ambavyo vilikuwa havijawahi kuonekana kabla wakati wanachunguza maambukizi ya magonjwa mengine.

Ingawa alisema kuwa majibu ya utafiti wake ulikataliwa kwa sababu hakuwa picha za ushahidi alizowasilisha ni sawa na virusi vya mafua ya kawaida.

Uzinduzi mpya wa B814 uiandikwa katika jarida la ' British Medical Journal' mwaka 1965 na picha ya kwanza ya kile ambacho alikiona iliweza kuchapishwa miaka miwili baadae kile alichoona kiliweza kuchapishwa katika jarida la ' General Virology '.

Kwa mujibu wa bwana Winter, anasema kuwa Dr Tyrrell na Dr Almeida, wakishirikiana na Prof Tony Waterson, mkuu wa St Thomas ambaye aliamua kuvipa jina virusi hivyo kuwa ni virusi vya corona kutokana na muonekano wake katika picha uko sawa na taji.

Dr Almeida baadae aliweza kutunukiwa shahada ya udaktari wa afya.

Baadae Dr Almeida alikuwa mwalimu wa yoga lakini alirejea tena katika majukumu yake ya Virology mwishoni mwa mwaka 1980 aliposaidia kupiga picha ya virusi vya Ukimwi katika kitabu.

June Almeida alifariki mwaka 2007, akiwa na miaka 77.

Miaka 13 baada ya kifo chake , ndio hatimaye kazi yake inatambuliwa na kueleweka duniani kote.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad