Maoni ya Wabunge Kuhusu Nani Kuwa Bingwa wa Ligi Tanzania Bara



Ligi Kuu Tanzania bara (VPL) imesimama kwa muda wa mwezi mmoja sasa kutokana janga la virusi vya Corona ambalo linaendelea kuithiri dunia, huku kukiwa hakuna mbadala wa hatma yake kutkana na hali hiyo.


Tangu Serikali ilipotangaza kusitisha shughuli zote za mikusanyiko ya watu nchini ikiwa ni pamoja na shughuli za michezo, Machi 15, kumekuwepo na mijadala mbalimbali juu ya namna nzuri ya kumaliza michezo iliyobakia ya ligi ili kumpata bingwa pamoja na wawakilishi wa michuano ya klabu barabi Afrika.

Katika kikao cha 15, mkutano wa 19 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baadhi ya Wabunge wametoa maoni yao kuhusu namna nzuri ya kumaliza ligi pamoja na kumpata bingwa wa ligi na wawakilishi wa Afrika.

Miongoni mwa Wabunge hao ni Mbunge wa Sengerema, Mhe. William Ngeleja ambaye amesema kuwa ni vyema Simba akatangazwa bingwa kutokana na mazingira tuliyo nayo pamoja na kigezo cha kuziacha timu zingine kwa pointi nyingi.

Kuhusu namna ya kumpata mwakilishi wa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika ambaye awali alikuwa akipatikana kutokana na michuano ya shirikisho 'Azam Sports Federation Cup', Mhe. Ngeleja amesema "kwa sababu mashindano yapo katika ngazi ya robo fainali, wanaweza kucheza wakiwa kwenye Karantini wakapata bingwa au mshindi wa pili ambaye ni Azam FC akapewa nafasi hiyo".

Naye Mbunge wa Chemba, Mhe. Juma Nkamia amesema kuwa kwakuwa michuano ya klabu barani Afrika itaanza tena mwezi Agosti, ni vyema timu inayoongoza ligi ikapewa ubingwa na timu inayoshika nafasi ya pili ikashiriki Kombe la Shirikisho.

Maoni hayo yamepingwa na wadau wengi wa soka nchini wakisema kuwa ni mapema kutoa hatma muda huu ikiwa nchi zote barani Afrika pamoja na Shirikisho la Soka Afrika CAF ziko katika harakati za kutafuta nafasi ya kumalizia kalenda zao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad