Chukua Hatua Hizi Kama Unataka Kuacha Ulevi wa POMBE..ni Ngumu ila ni Kwa Faida yako



Mkuu kabla ya kuamua kuacha kunywa pombe kuna maswali ya awali ya kujiuliza.

1. Kwa nini unataka kuacha kunywa pombe? Watu wanaacha kwa sababu mbalimbali kama ukata etc.
2. Mambo gani mazuri yanatokana na wewe kunywa pombe? Muhimu kujua ili kutafuta njia mbadala baada ya kuacha.
3. Mambo gani mabaya yanayotokana na wewe kunywa pombe?
4. Mambo gani mazuri unayategemea baada ya kuacha kunywa pombe?
5. Mambo gani mabaya yanayoweza kutokana na wewe kuacha kunywa pombe?

Kutokana na majibu ya maswali hapo juu, hizi ni baadhi ya hatua unazoweza kuchukua. Zipo nyingi. Hizi ni baadhi tuu.

1. Kama ni mnywaji sana ongea kwanza na daktari wako. Kuacha pombe ghafla kunaweza kukuletea madhara hasa kama ni mnywaji sana. Kuacha ghafla unaweza ku-suffer from panic attacks, anxiety, shakes, mapigo ya moyo kwenda mbio, au hata mwili kupungua. Kwa hiyo, kunaweza kuwa na umuhimu wa kupata ushauri wa kitaalamu kwanza jinsi ya kuacha.

2. Badilisha attitude yako juu ya pombe. Kumbuka hakuna anayekulazimisha kuacha pombe (rafiki yako mkubwa ambae amekuwa na wewe kwa muda mrefu). Panga tarehe za kuacha. Be ambitious but reasonable. Kama ni mnywaji sana punguza kidogo kidogo. Ukiacha gafla unawezapatwa na symptoms. Ndio maana wanasizitiza kupata ushauri wa daktari ili aweze kukupangia kitaalamu jinsi ya kuacha pombe.

3. Kama una pombe nyumbani, get rid all of them. Unaweza kusema itabidi uache pombe kidogo kwa ajili ya wageni. Lakini it is perfectly fine kumpa mgeni chai, soda au hata maji. Kama ni mgeni aliyezoea kuja kwako na kunywa pombe ukimwambia kuwa huna pombe ndani kwa sababu una mkakati wa kuacha kunywa, nadhani atakuelewa vyema.

4. Rudi back to your feelings. Ukijiskia unataka kulia, then lia. Laugh when you can. Kula ukiwa na njaa. Lala ukiwa umechoka. Usitumie ule muda uliokuwa unautumia kunywa pombe kwa kwenda kulala. It won't help. Mwanzoni itaonekana ni weird but embrace it. Kuna uwezekano kwa sababu ya pombe hujawahi kujua hisia zako kwa muda mrefu. So, you will have to learn to curve.

5. Usifanye kitu ambacho hauko tayari kukifanya. Kama unaenda kwenye sherehe na kuna pombe usinywe pombe kwa sababu wengine wanakunywa. Mwanzoni inaweza kuwa ngumu lakini you will need to rain check. Protecting your sobriety should be your first priority.

6. Kuna uwezekano mkubwa wa kuachana kwa muda na baadhi ya marafiki zako ambao ulikuwa unakunywa nao. Baadae utakuja kushangaa kuwa in fact marafiki ambao ulikuwa unakunywa nao walikuwa wanakunywa only occasionally, tena bia mbili tuu wakati wewe ulikuwa ulikuwa unakata bia tano.

7. Kama nyumbani unatumia viungo vya kupikia ambavyo vinalazimisha kuwepo kwa bia au wine, then achana navyo. Pia kuna wale wanaosema nyamba choma haiendi bila bia. Itakubidi ukae mabli na nyama choma kwa muda. Wapo ambao wanachoma nyama na kuichanganya na bia wakati inachomwa. Itabidi uache kama unafanya hivyo.

8. Tafuta kibox kidogo cha mbao cha kuhifadhia fedha. Kila unapofikiria kununua pombe, chukua hizo pesa na tumbukiza huko. Baadae utakujashangaa kiasi cha fedha ambazo ulikuwa unapotezea kwenye pombe. Ikishindikana basi tumia hizo fedha kupunguza stress kama kupata massage au jiunge na gym.

9. Nununua ring ya bei rahisi na ivae kila wakati kama kielelezo kuwa haugusi tena pombe. Kama wewe ni Mkatoliki unaweza kuvaa Rozari kama kielelezo kuwa hutakunywa pombe wakati ukiwa umeivaa. Ukisikia hamu ya pombe tuu look at the ring.

10. Kunywa maji kwa wingi. Hata kama ni kutembea na chupa za maji barabarani usiogope.

11. Omba support kutoka kwa ndugu mme/mke kuhusu what you are going through and nini unachotaka ku-achieve.

12. Kama kuna chama chochote cha watu wanaotaka kuacha pombe, jiunge nacho. Kama ukikuta chama chenyewe hakina mshiko, don't feel guilty. Its not your fault.

13. Baada ya siku 90 ya kuwa sober, your whole outlook itabadilika na mwili wako utakuwa in full recovery mode. Utakuwa mtu tofauti na ulivyokuwa na kuna uwezekano weight yako ikapungua pia. Don't worry.

14. Tengeneza list ya vitu ambavyo umefanya by using alcohol without alcohol, then celebrate maana list itakuwa ndefu.

15. Furahia how it feel unapokwenda kulala jioni bila kupoteza network.

16. Usijaribu kuwaelezea watu kuhusu kuacha kwako pombe. Watu wengi hawanywi pombe kama walivyokuwa wanakinywa zamani. Hawapo kama wewe na hawataweza kukuelewa kuwa una tatizo la kunywa pombe. Of course, wako ambao wana hilo tatizo. Either way kuna uwezekano wakakuambia huna tatizo. Mtu akitaka kukukaribisha pombe mwambie asante lakini nitakunywa soda; najaribu kupunguza weight. Kama ni watu wa karibu ipo siku watajua kweli wata-appreciate kwa wewe kuamua kuachana na pombe.

17. Kubali na kumbuka kuwa pombe sio kitu muhimu maishani mwako kupita vyote.

18. Kuwa na sababu nzuri ya kuacha pombe. Ni muhimu sana kuwa na sababu tena iwe ya msingi. Kama sababu ni pesa imepungua, kuna uwezakano ukarudia tena pombe kama pesa ikiongezeka. So ni bora kuwa na strong and valid reason.

18. Usikwepe kwenda sehmu ambazo utakunywa pombe, kama kwenye sherehe, n.k. Badala yake nenda kwenye hizo sehemu ukiwa na attitude nzuri na kumbuka kuwa na good time bila hata kunywa pombe. You can have a good time bila kunywa pombe. Yes, you can. Tena utashangaa jinsi watu na heshima zao wanavyo-behave baada ya kulewa. Kwangu hii ndio sababu pekee iliyonifanya nisinywe pombe.

19. Memorise a prayer, shairi, nk then rudia kulisema pale unapokuwa katika hatihati za ku-loose your control. It will keep your heard together. Kwa mfabo mtu ambaye anataka kuacha kuchukua rushwa anaweza ku-memorise baadhi ya sentensi kwenye speeches za Mwalimu Nyerere kama "Rushwa ni adui wa haki." Tafuta misemo ambayo inahusina na ulevi.

20. Jipe mwenyewe zawadi kila siku au kila saa kwa kutokunywa. Sio lazima iwe zawadi kubwa. Just a simple treat kujipongeza.

21. Nasistiza tena. Ongea na daktari wako. Kuacha pombe gafla kunaweza kukuletea madhara makubwa hasa kama ni mnywaji wa kupindukia.

22. Fanya mazoezi. Mazoezi yatakufanya u-deal the stress na pia yatasaidia kutuliza ubongo wako na kuboresha afya yako kwa ujumla.

23. Kulingana na ushauri wa daktari, meza vitamin B supplements kila siku kwa wiki ya kwanza ya kuacha pombe. Pombe inaadhiri uwezo wa mwili wako ku-absorb these. Upungufu wa Vitamin B unaweza kusababisha severe cognitive impairment. So, ongea na daktari wako juu ya hili na hasa kama unatumia medication nyingine.

24. Kama ni mlevi sana jaribu ku-visualize jinsi unaakavyokuwa wakati ukiwa umelewa na jiulize kama unataka kuendelea kuwa vile.

25. Kama unatoka kazini na kwenda moja kwa moja bar kunywa, jaribu kubadilisha routine kwa kufanya shughuli nyingine kama kutembelea ndugu na jamaa, kwenda gym au kanisani/msikitini. Ikishindikana kabisa then, jikite JF. JF is never boring na utafaidika zaidi ya kunywa pombe. Ni heri uwe mlevi ya JF kuliko mlevi wa pombe.

26. Kula kwanza kabla ya kunywa. Hii itapunguza interest ya kutaka kunywa.

27. Siku za mwanzoni punguza kiasi cha pombe unayokunywa. Halafu jaribu ku-imagine kutokana na kunywa mno jinsi unvyopoteza network, unavyojitapikia, kichwa kinauma, unachelewa kazini, nk.

28. Don't give up. Wapo wanaosema wamekuwa wakinywa kwa muda mrefu sana kwa hiyo hawawezi kuacha, sijui wamejaribu kuacha mara nyingi lakini nimeshindwa, n.k. Hakuna age limit ya kuacha kunywa pombe. Unaweza kuacha katika umri wowote. It is never too late to quit drinking.

29. Kama wewe ni mtu wa club sana, kuna strategy alikuwa anatumia rafiki yangu na ilimsadia. Kuwa yeye atakuwa dereva kila tukienda out. Kwa hiyo hatagusa pombe kabisa ili aturudishe nyumani salama. Ilimsaidia sana kutokunywa.

29. Kumbuka kuacha kunywa pombe kutakuongezea urefu wa maisha yako hapa duniani. Pamoja na magojwa yanayosababishwa directly na unywaji wa pombe kupita kiasi, ukiwa mlevi kupindukia unaweza kufanya mmabo ya ajabu na kusabisha sio kifo chako tuu bali vifo kwa watu wengine pia kama ku-drive wakati umelewa.

30. Don't let guilty affect you. Unaweza kuji-feel mshamba au guilty kwa kutokunywa pombe lakini usilaumu mwenyewe au mtu mwingine. Hakuna kitu muhimu kama wewe. You are of no use to anyone kama ukifa na magonjwa yanayosabishwa na ulevi. You must overthrow the oppressive rule of alcohol and start afresh, just as any country in revolution. Jiulize Libya waliweza kuachana na Gadaffi wewe kweli utashindwa kuachana na pombe? It will be hard and you must learn from the past, lakini kumbuka kuwa umenganywa na pombe kwa muda mrefu. Sasa ni muda wa kuanza kuyaishi maisha yako. Those around you will appreciate it too.

Goodluck.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad