Afariki Baada ya Kukimbizwa na Polisi Kwa Kukosa Maski


Mwanamume mmoja katika kaunti ya Makueni eneo la Kibwezi amefariki baada ya kutumbukia kwenye kidimbwi cha samaki alipokuwa anakimbia maafisa wa polisi baada ya kukosa maski.

Kisa hicho kimetokea katika kijiji cha Kambu na inadaiwa kuwa jamaa huyo alikuwa anakwepa mkono wa sheria kwa kukosa kuvalia barakoa kama ilivyopendekezwa na serikali.

Yanajiri haya huku gavana wa kaunti ya Kakamega Wyclife Oparanya akiwaonya wakaazi wa kaunti hiyo dhidi ya kutembea maeneoa ya umma bila barakoa.

Oparanya amesema maafisa wa polisi kaunti hiyo wako ange kuona atakayekiuka amri hiyo na kuongeza kuwa hakuna mtu yeyote atakayesazwa katika mchakato huo.

Wakenya hawana maskio kamwe! Watu 25 watiwa nguvuni wakinywa mvinyo

Amri ya kuvalia maski nchini ilitagazwa wazi na mkuu wa polisi Hillary Mutyambai ambaye alisema ni sharti kila mkenya kuvalia barakoa ili kuepuka adhabu ya kulipa shilingi alfu 20,000 ama kufungwa gerezani

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad