Ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka na kulawiti mwanae wa kumzaa



Na Amiri kilagalila,Njombe
Mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Njombe imemuhukumu Hezron Ndone ( 44) mkazi wa joshoni kata ya mji mwema mjini Njombe  kwenda jela  kifungo cha maisha kwa kosa kumbaka na kumlawiti  mtoto wake wa kumzaa ambaye ni mwanafunzi darasa la tano  mwenye umri wa miaka 10.

Akisoma hukumu ya kesi namba 14 ya mwaka 2020  hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya mkoa Njombe Hassan Mkakube alisema mtuhumiwa alishtakiwa kwa makosa manne mawili ya kuzini na maalimu  kinyume na kifungu cha sheria namba 158 kifungu kidogo cha kwanza na  makosa mawili ya kulawiti kinyume na kifungu namba 54 kifungu kidogo cha pili na cha kwanza  vikisomwa pamoja na kifungu namba 185 cha sheria ya mtoto.

Hakimu Makube alisema kupitia mashahidi watatu kati ya sita wa upande wa mashtaka akiwemo shahidi namba moja ambaye ni mke wa mshtakiwa , shahidi namba mbili ambaye ni mtoto aliye athirika pamoja na shahidi namba tatu ambaye ni daktari aliyefanya vipimo vya mtoto mahakama imejiridhisha kuwa mshtakiwa kwa nyakati tofauti alizini na kumwingilia kinyume na maumbile mtoto wake mwenye umri wa miaka 10.

Hakimu Hassan Makube alisema shahidi namba moja ambaye ni mke wa mshtakiwa Valentina Mkorongo aliieleza mahakama  kuwa awali alikuwa na mgogoro na mume wake na ikatokea akawa analala jikoni na mtoto wake mdogo huku watoto wake wengine wanne wakilala chumbani na baba yao akiwemo binti yake wa kike.

Shahidi namba mbili ambaye ndiye muathirika aliieleza mahakama kuwa akiwa na wadogo zake watatu baba yake alikuwa anawalaza wadogo zake kitandani na yeye alikuwa akilala na baba yake kwenye godolo lililokuwa likitandikwa chini na hapo ndipo baba yake alipokuwa akimvua nguo na kumwingilia kwa zaidi ya mara saba.

Makube alisema shahidi namba sita ambaye ni mdodgo wake na muathirika aliieleza mahakama kuwa yeye alikua akilala na wadogo zake kitandani lakini dada yao mkubwa alikua akilala chini na baba yao.

Hakimu Hassan Makube alisema mahakama ilisikiliza ushahidi wa daktari aliyemfanyia uchunguzi muathirika na kuthibitisha kuwa mtoto hakuwa na bikira na sehemu yake ya nyuma ilikuwa imeingiliwa na baadaye akajaza fomu namba tatu kwa ajili ya hatua nyingine.

Mshtakiwa ambaye alikuwa akitetewa na wakili Emmanuel Chengula alipewa nafasi ya kujitetea ambapo alikataa kutenda kosa na kuieleza mahakama kuwa huenda waliomwingilia binti yake ni vijana ambao amewahi kuwahisi kuwa na uhusiano na binti yake.

Hata hivyo wakili wa serikali Andrew Mandwa akiwa naye  Happines Makungu,Nura Minja waliiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili iwe fundisho kwa wengine wanaothubutu kufanya vitendo vya namna hiyo.

Baada ya mahakama kuridhika na maelezo ya mashahidi  imemkuta mtuhumiwa na makosa na kumhukumu miaka 30 kwenda jela kwa kosa la kuzini na binti yake na kifungo cha maisha kwa kosa la kumwingilia kinyume na maumbile pamoja na kutoa fidia ya shilingi milioni 10 ikiwa ni fidia kwa muathirika.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kwanini DNA isitumike?! Mama anasema ana ugomvi ns mumewe, je hawezi kumsingizia baba huyu,? Ushahidi udio na evidence ya kutosha, hautoshi kuamua kesi kwa haki

    ReplyDelete
  2. Mtoto anaweza kufundishwa na mama ili kumtia Haitiani baba. Haki itendeke!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad