Aibu ya Maski! Cyril Ramaphosa Ashindwa Kuvalia Maski Akiwa Moja kwa Moja Kwenye Runinga
0
April 24, 2020
Katika malimwengu ya maisha ya kiafrika kama unafanya kazi hospitalini ama kama wewe ni mtu wa kufanya kazi ya mjengo swala la kuvalia barakoa ama maski si geni kwako ,japo kwa wale walioanza kuvalia vitambaa hivyo kwa mara ya kwanza wanapitia katika changamoto si haba.
Hata hivyo mlipuko wa virusi vya corona ulimwenguni umebadili maisha ya wengi na kuwalazimu kujikinga kwa kununua barakoa na kuzivalia.Wakiongozwa na rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa ambaye alikuwa moja kwa moja kwa televisheni alijipata pabaya baada ya barakoa aliyokuwa anajaribu ili kuwaonyesha wananchi wa taifa namna ya kuzivalia zao ,kusumbukana kuivalia na kuzua mdahalo mkubwa.
Katika video ambayo imekuwa ikienea kwenye mitandao ya kijamii,Ramaphosa alisumbukana kwa dakika zaidi ya moja akijaribu kuivaa barakoa hiyo.
Tazama picha hizi.
Cyril Ramaphosa tried to wear his face mask on live TV and it did not ...
Kulingana na wananchi wa Afrika Kusini na walioshuhudiwa kisa hivo walidai huenda kichwa cha Ramaphosa kilikuwa kikubwa na hivyo maski hiyo haingemtoshea.
Wengine walidai kuwa huenda kiongozi huyo alikuwa anajaribu kuficha tu macho yake kwani kibarakoa alichokuwa anakivalia hakingesetiri ukubwa wa kichwa chake.
Kwa sasa mataifa mengi ulimwenguni yamewahimiza wananchi wake kuvalia maski kwani ndio njia ya kipekee ambaypo inaweza kuzuiya maambukizi zaidi .
Kwa sasa mataifa zaidi ya 200 ulimwenguni yamedhibitisha kuwepo kwa virusi vya corona na kwa mujibu wa WHO watu takriban 2.64 wanaripotiwa kuambukizwa virusi hivyo.
Tags