Ajali ya Mkuranga Rais Magufuli Atuma Salamu za Rambirambi, Asema inauma Sana


Rais John Magufuli ametuma salama za rambirambi kwa ndugu jamaa na marafiki wa watu 18 walipoteza maisha katika ajali iliyotokea leo Aprili 15 eneo la la Kilimahewa, Mkuranga.

Katika ajali hiyo iliyotokea alfajiri ya leo ilihusisha gari aina ya Costa na roli la mizigo aina ya Scania ambapo magari hayo yaligongama uso kwa uso.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya mawasiliano ya Rais Ikulu, Magufuli amemtuma Mkuu wa mkoa wa Pwani kumfikishia salama hizo kwa familia zilizopoteza ndugu.

“Ninawaombea familia za marehemu wote ndugu jamaa na marafiki kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki cha majonzi ya kuwapoteza watanzania wenzetu kwa idadi kubwa namna hii inauma sana,”.

Amevitaka vyombo vya usalama barabarani kuhakikisha vinachukua hatua madhubuti kudhibiti ajali.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad