Supa Nyamwela ameeleza hayo baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba Ali Choki amekimbia hapa Dar Es Salaam na kukimbilia Jijini Mwanza kwa sababu ya matatizo yake ya kiafya.
"Ndugu yangu Ali Choki yupo kama kawaida bali ameamua kubadilisha upepo na maisha kwa kuishi jijini Mwanza, naweza kukiri kwamba ni kweli alikuwa anaumwa kwa kipindi kirefu lakini sasa hivi mwili wake umerudi, yupo sawa, amerudisha afya yake, na anaendelea na kazi" amesema Supa Nyamwela
Aidha Supa Nyamwela ameongeza kusema "Siwezi kusema alikuwa anaumwa nini ila Tanzania na Dunia ijue tu Ali Choki yupo sawa na amerudi kuliko yule wa zamani"