KAMPUNI ya simu za mkononi ya TECNO inatarajia kuandika historia Tanzania kwa kuzindua simu yake mpya ya CAMON15 Aprili 15 mwaka huu kwa kutumia mitandao ya kijamii yaani ‘Online Launch’
.
Akizungumzia kuhusu uzinduzi huo katika ofisi za TECNO jiijini Dar es Salaam leo afisa masoko wa TECNO mtandaoni, Salma Shafi amesema hii ni fursa kwa kampuni hiyo kuwasiliana na wateja wake na Watanzania wote kwa ujumla kupitia teknolojia ya intanteti.
“Hii sio tu nafasi nzuri kwa TECNO kuwasiliana na wateja wetu na Watanzania moja kwa moja, lakini pia inamaanisha kuwa matumizi ya vifaa vya kielektroniki na teknolojia Tanzania yanakuja katika hatua mpya sawa na simu tutakayoizindua CAMON15 ambayo ina teknolojia mpya ya kisasa kabisa ambapo wateja wetu wataweza kushuhudia uzuri wake” amesema Salma.
Wakati wa uzinduzi huo TECNO itatambulisha rasmi toleo la simu yake mpya ya CAMON15 pamoja na teknolojia yake ya kisasa iliyotumika kutengeneza kamera hiyo pamoja na sifa nyinginezo.
Mwonekano wa TECNO CAMON 15
TECNO ambayo ni kampuni kinara yenye teknolojia ya juu katika tasnia ya smartphone, imekuwa kipaumbele katika kuwapandisha viwango wateja wake kwa kutoa matoleo mbalimbali ya simu zake kulingana na mahitaji.
Hata hivyo toleo hilo mpya la CAMON15, kampuni hiyo imeweka kamera yenye MP64 nyuma huku ikisaidiwa na kamera nyingine ndogo mbili ili kuongeza ufanisi zaidi katika suala la picha.
Kamera ya TECNO CAMON15 ina teknolojia iliyojikita katika kutatua changamoto za kupiga picha kwenye maeneo yenye mwanga hafifu au usiku. Kamera hii imeondoa ama imejengewa uwezo wa kuvikabili vizuizi vyote ambavyo hufifisha picha, kutokana na teknolojia hii, picha iliyopigwa na CAMON15 inabaki kuwa bora hata ikikuzwa (zoomed) mara 8.
Fuatilia uzinduzi huo wa CAMON15 utakaofanywa na TECNO siku ya Jumatano Aprili 15, unaweza kufuatilia katika kurasa za TECNO Facebook, Instagram, Twitter, Tik Tok TECNO Mobile Tanzania.