Ali Kiba Afunguka Uhusiano wake na Hamisa, ‘Nampenda Mobetto’
0
April 09, 2020
Ali Kiba ameeleza uhusiano uliopo kati yake na mrembo, Hamisa Mobeto ambaye ni mama wa mtoto wa Diamond Platinumz.
King Kiba ambaye leo, Aprili 8, 2020 ameachia video ya wimbo wake mpya ‘Dodo’ huku Hamisa akiwa mrimbwende nyota wa video hiyo (video vixen), amesema kuwa anamchukulia kama msichana anayemheshimu na anampenda.
“Mimi na Hamisa ni kama familia, namheshimu… ni msichana ambaye anajiheshimu na ninampenda,” Ali Kiba alijibu maswali ya Sound Brown wa Clouds Fm.
Aliongeza kuwa anamkubali Hamisa kwakuwa anajielewa na kwamba kwake kufanya kazi naye sio kitu kibaya.
“Watu waliweka dot kuwa kwakuwa Hamisa yuko Verde [Zanzibar] na Ali Kiba naye yuko Verde kwahiyo watakuwa wana-Verdeana, hapana. Ile ni hotel ya Kimataifa, na Hamisa ni wa Kimataifa na Ali naye ni wa Kimataifa kwahiyo watu wa Kimataifa walikutana,” aliongeza.
Kiba na Hamisa wanaonekana kwenye video ya ‘Dodo’, ambapo Ali Kiba anamuimbia mwali wake mwenye hadhi ya ‘Dodo’ la Kifalme, akimsimu mama yake kwa kumleta duniani na kumpa malezi.
Video ya wimbo huo imepata mapokezi mazuri ikifanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye ‘trending’ ndani ya saa chache.
Tags