Ali Kiba Awekwa Kiti Moto Katikati ya Hamisa Mobetto na Tanasha....Mwenye Amchagua Hamisa Mobetto


Mkali wa BongoFleva Alikiba amesema kama utamletea Hamisa Mobetto na Tanasha Dona ili mmoja wapo awe "video queen" kwenye kichupa chake basi atamchagua mrembo Hamisa na atamuacha Tanasha.


Alikiba tayari ameshafanya kazi na Hamisa Mobetto katika video ya wimbo wake mpya wa dodo, pia aliwahi kufanya kazi na mrembo Tanasha Donna mwaka 2015, katika wimbo wa nagharamia ambao alishirikiana na Christian Bella.

Akieleza hayo kwenye show ya Friday Night Live ya East Africa Tv, inayoruka kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 hadi 5:00 usiku  Alikiba amesema   "Mimi na Hamisa tumekutana location,  menejimenti yangu ndiyo iliandaa kila kitu, kila mmoja alienda kivyake Zanzibar, hatukwenda pamoja na ukiniletea Hamisa Mobetto na Tanasha, namchagua Hamisa kuwa video queen kwenye video yangu".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad