Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema amehoji mgonjwa wa Mwanza aliyekutwa na virusi vya Corona ndani ya siku tano alikuwa wapi.
“@umwalimu taarifa yako inasema mgonjwa mmoja mkazi wa Mwanza aliwasili kutoka Dubai tarehe 24 Machi na aligundulika tarehe 29 Machi,” aliandika Lema katika ukurasa wake wa Twitter.
“Siku hizi 5 alikuwa wapi? Tanzania itaumia sana hapo mbele kuliko nchi yoyote,” aliandika Lema.
Lema amesema Virusi vya Corona vinaweza kuiangamiza nchi, Mungu hapendi uzembe
@umwalimu Taarifa yako inasema mgonjwa mmoja mkazi wa Mwanza aliwasili kutoka Dubai tar 24 Machi na aligundilika tarehe 29 Machi akiwa Mwanza.Siku hizi 5 alikuwa wapi?Tanzania itaumia sana hapo mbele kuliko Nchi yoyote,Corona virus inaweza kuangamiza Nchi.Mungu hapendi uzembe.— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) April 6, 2020