Askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) kikosi cha KJ 843, Wilaya ya Nachingwea, mkoani Lindi, Shabani Mkondya (34) amehukumiwa kifungo cha miaka 3 Gerezani, baada ya kukutwa na hatia ya kumjeruhi mkazi wa Kata ya Nyangao, Ramadhani Mussa, kutokana na wivu wa kimapenzi.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu mkazi mwandamizi wa Mahakama hiyo, Maria Batraine, baada kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.
Kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mshitakiwa alipewa nafasi ya kujitetea,na kuiomba Mahakama isimpe adhabu kali kwa madai ni mkosaji wa mara ya kwanza na pia alilazimika kufanya hivyo baada ya kutingwa na hasira kutokana na kitendo alichofanyiwa na mlalamikaji wake.
"Naoimba Mahakama tukufu isinipe adhabu kali,kwani ilinilazimu kufanya hivyo kutokana na hasira baada ya kumfumania mlalamikaji akivuruga uchumba wetu " Alijitetea Coplo Mkondya.
Sikuwahi Kudhania Kuna Siku MSICHANA wangu wa Kazi Atanibaka. Nimeumizwa Sana
Baada ya utetezi huo, Hakimu Batraine alimuuliza mwanasheria, Emmanuel John, iwapo ana kumbukumbu makosa ya zamani kwa mshitakiwa na kujibu hana, lakini aliomba adhabu kali itolewe kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia ya aina hiyo, ikizingatiwa yeye ni mlinzi wa umma.
Hakimu Betraine akitoa hukumu katika kesi hiyo namba 61/2019, kupitia kifungu cha Sheria namba 225 kanuni ya adhabu sura ya 16/2002, alisema amesikia maombi ya pande zote mbili, na kumuhukumu kifungo cha miaka mitatu Gerezani.