Askofu wa Kanisa la Ufufuo na uzima Josephat Gwajima amesema kuwa ameomba radhi kwa wananchi wa DRC Congo mara baada ya kutoa kauli ya kukashifu nchi hiyo kwa kile alichodai kuwa nchi hiyo imekubari kufanyiwa majaribio ya chanjo ya Covid 19.
Gwajima alitoa mahubiri ya kukemea kitendo hicho siku chache tuu baada ya umoja wa madaktari kutoka nchini ufaransa kusema kuwa itaanza kufanya majaribio ya chanjo za Corona. Gwajima amesema alipewa taarifa zisizo sahihi kabla ya mahubiri yake.
“Niliwaomba msamaha wakongo maana kabla ya ibada niliambiwa kuwa Kongo wameshaanza majaribio nikasema kwenye ibada lakini baadaye nikajua ukweli kwamba hakuna majaribio yoyote yale nikapiga simu kwa wakongo,” amsema Gwajima.