Aunt Apata Kigugumizi Kuachana Tena Na Iyobo



BAADA ya tetesi kuzagaa kuwa ameachana na mzazi mwenzake, Moses Iyobo ‘Moze’, staa wa Bongo Movies, Aunt Ezekiel amepata kigugumizi na kusema watu waachane na habari hizo kwani kwa sasa habari ya mjini ni Corona tu.

Akipiga stori na OVER ZE WEEKEND, Aunt alisema hawezi kuzungumza chochote kuhusu kuachana na Iyobo badala yake kila mtu anatakiwa awe makini na kujua jinsi ya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona vinavyosababisha homa kali ya mapafu ya COVID-19.

“Huu siyo wakati wa kujadili vitu visivyokuwa na tija kwa jamii, ishu yangu na Mose haina faida yoyote hivyo watu wanavyojua wajue hivyohivyo maana sina muda wa kuzungumza hayo maana sasa hivi tuko kwenye janga kubwa la Corona,” amesema Aunt.

Aunt na Mose wanadaiwa kutengana tena kwa awamu ya pili ikiwa ni baada ya kurudiana miezi michache iliyopita.

STORI: IMELDA MTEMA

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad