Baada ya lock down ya wiki kadhaa, sasa rasmi Wuhan,China imeanza kuruhusu Watu kusafiri kutoka eneo hilo ambalo linaaminika kuwa kitovu cha virusi vya corona hii ni baada ya maambukizi kupungua, Watu wamefurahia wakisema sasa ni muda wa kuonana na familia zao baada ya kulazimika kubakia Wuhan kwa muda kupisha corona.
Hadi takwimu za asubuhi hii China ina vifo vya corona 3333, wagonjwa ni 81,805 na idadi ya wanaopona imepanda hadi 77,290.