Baada ya Mrembo Nicole Kumpa TAMU Harmonize..Sarah Ajirudi na Kukubali Yaishe



Moshi mweupe! Mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Rajab Abdul ‘Harmonize’, Sarah Michelotti amefufua matumani ya wawili hao kurudiana kufuatia kitendo chake cha kujirudi na kumtumia mwenzi wake huyo ujumbe mtamu wa kimahaba.

Sarah ambaye ni raia wa Italia na Harmonize au Harmo, wiki iliyopita waliingia kwenye mgogo mkubwa wa kimapenzi kwa tuhuma za usaliti.

Sarah alidaiwa kumtuhumu Harmo kusaliti penzi lao kwa kulala na video queen matata Bongo, Nicole Joyce Berry ambaye amemtumia kwenye video yake ya Wimbo wa Bedroom.

Sarah alidaiwa kutinga nyumbani kwa Nicole maeneo ya Mbezi-Beach jijini Dar kisha kufanya fujo akimtuhumu mrembo huyo kutembea na Harmo.

Nicole alidaiwa kumpa ‘tamu’ bosi huyo wa Lebo ya Konde Music Worldwide walipokuwa wakishuti video ya Wimbo wa Bedroom.Hata hivyo, inaonekana mambo yameanza kukaa vizuri baada ya Sarah kumaliza hasira zake na kuanza kufuta zile tetesi kwamba wameachana.

Kupitia Insta Story kwenye ukurasa wake wa Instagram, Sarah alitupia picha ya Harmo akipafomu jukwaani na kuandika;“Mume gharama zaidi wa moyo wangu.

Wakati wote hukosei baby harmonize_tz”Pamoja na hayo, lakini bado wawili hao hawajarejesha ufuasi wa kila mmoja kwenye kurasa zao za Instagram baada ya kuondoana wiki iliyopita hivyo kuendeleza sintofahamu juu ya uhusiano wao.

Stori:NEEMA ADRIAN, Ijuma

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad