Baada ya Tanasha Kufanyiwa Sinema na Kusepa Kwao....Unaambiwa Mondi na Zari Mambo Ng'are ng'are



BAADA ya kudumu kuishi bila mawasiliano kwa zaidi ya miaka miwili, zilipendwa wawili, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ na Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’, sasa wanatajwa kuwa kwenye hali nzuri ya kimawasiliano, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linakupa mchapo kamili.

TUWASIKILIZE WATU WA KARIBU

Kwa nyakati tofauti, watu wa karibu wa familia ya Mondi ambao wameomba hifadhi ya jina, wameeleza kuwa, wawili hao kwa sasa wameanza kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa takriban miaka miwili. “Sasa hivi mambo safi, wameanza kuwasiliana na mambo yanaonekana si kama zamani. Si unajua zamani ilikuwa kuwashiana fulu ileile, no kusemeshana kabisa,” alisema mmoja wa watu hao.


NI BAADA YA KUACHANA NA TANASHA…

Mwingine aliongeza kuwa, uhusiano huo umezidi kupamba moto zaidi katika kipindi hiki ambacho Mondi amemwagana na mzazi mwenzake, Tanasha Donna ambaye amerudi mazima nyumbani kwao nchini Kenya.

“Jamaa kazidisha zaidi mawasiliano na Zari baada ya kuona maji yamemwagika kwa Tanasha na ukizingatia kati ya watu ambao Mondi aliamini anaweza kuwa mke ni Zari,” alisema.

JITIHADA SI ZA KITOTO

Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linafahamu kwamba, licha ya Mondi kutokuwa na mawasiliano mazuri na Zari kwa muda mrefu, lakini wapo baadhi ya watu kwenye familia ya Mondi ambao wamekuwa wakiwasiliana na mwanamama huyo mara kwa mara huku pia wakitamani arejee kwenye himaya yake.

Jitihada za kumpata Mondi ili aweze kuzungumzia ishu hiyo hazikuzaa matunda kufuatia simu yake ya mkononi kuita bila kupokelewa, lakini hata hivyo, mtu wa ndani ya familia hiyo amedai habari zina ukweli kwa asilimia mia moja.

BABA MONDI AMEKUWA AKITAMANI

Baba mzazi wa Mondi, Abdul Juma ‘Baba D’ amekaririwa kwa nyakati tofauti na Magazeti Pendwa ya Global akisema, anatamani kumuona Mondi anamaliza tofauti zake na Zari ili waweze pia kuwalea watoto wao vizuri.


ZARI AANIKA MWANGA MPYA

Kupitia Mtandao wa TikTok, mwishoni mwa wiki iliyopita, Zari alitupia kipande cha video na kutamka kuwa amepokea ujumbe kutoka kwa zilipendwa wake japo hakumtaja, lakini wengi walijiongeza kuwa ni Mondi ambaye ni staa mkubwa wa muziki barani Afrika.

“I got a text from my ex the other day saying he was missing me. I said sorry, i can’t talk right now i’m a funeral. He said omg who is dead? I said my feeling for you did,” alisema Zari akimaanisha amepokea ujumbe kutoka kwa mpenzi wake wa zamani akimwambia kuwa amemmisi, huku Zari akionesha kama hataki-anataka fulani hivi.


MTAALAM ANENA

Mtaalam wa Saikolojia na Uhusiano, Joseph Shaluwa alizungumza na Gazeti la IJUMAA WIKIENDA na kusema, kitendo cha Mondi kuanza kuwasiliana na Zari na bibie huyo kutoa ushirikiano wa kujibu, kinaashiria kwamba sasa hasira na chuki kati yao zimeisha.

“Kama walikuwa hawasalimiani, ilisemekana pia Zari alikuwa hataki hata watoto wawasiliane na Mondi, hiki kinachoendelea sasa kinaonesha wawili hawa hawana tena kile kinyongo cha awali. “Unajua mtu hata kama mmeachana naye kwa ugomvi, kuna wakati tu utafika hamuwezi kuona umuhimu wa kuwa na kinyongo. “Mtarejesha uhusiano wa kawaida kwa ajili pia ya kuwaweka watoto wenu karibu na kuwalea vizuri,” alisema Shaluwa.


TUJIKUMBUSHE

Zari ambaye ni raia wa Uganda mwenye maskani yake Durban, Afrika Kusini na Mondi walimwagana Februari 14, 2018 baada ya mrembo huyo aliyezaa naye watoto wawili. Tiffah Dangote na Nillan kuandika ‘bonge la waraka’ kumtuhumu Mondi kuwa amekuwa na vitendo vinavyomvunjia heshima na hadhi yake katika jamii.

Tangu wamwagane, Mondi hakuwa na mawasiliano mazuri na mama watoto wake huyo hadi akaanzisha uhusiano mpya na Tanasha ambaye naye wamekuja kumwagana akiwa amezaa naye mtoto mmoja wa kiume, Naseeb Junior.

Source: GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad