Baba Mzazi wa Rihana Akutwa na Virusi vya Corona



Baba Mzazi wa msanii Rihanna, Ronald Fenty amekutwa na maambukizi ya virusi ya corona. Imeelezwa.

Kwa mujibu wa taarifa, Mzazi huyo wa Rihanna alifikishwa Hospitali baada ya kuonesha dalili nyingi za ugonjwa huo, kwasasa anaendelea vizuri na anapokea matibabu kwenye hospitali moja huko Barbados.

Mzee Ronald Fenty kwenye mahojiano yake na Gazeti la The Sun, amemshukuru mtoto wake, Rihanna ambaye amemsaidia kwa kiasi kikubwa kupata nafuu.

Pia mzee huyo ameweka wazi kuwa mbali ya binti yake ambaye amewahi kumburuza Mahakamani siku za nyuma amekuwa akimpigia simu kila siku kumjulia hali na vile vile alimnunulia mashine ya kusaidia kupumua "Ventilator" wakati hali yake haijakaa sawa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad