Barnaba "Nimepitia Maumivu na Machungu Mengi Mpango Wangu ni Kufuta Tattoo yake"

Msanii wa bongo fleva, Elias Barnaba maarufu Barnaba amesema mpango wake aliokuwa nao kwa sasa ni kufuta tattoo ya mama mtoto wake anayeitwa Zuu Namella ambayo ameichoro mkononi mwake.

Akiiambia WasafiTv, Barnaba alisema kama mtu akiachana na mpenzi wake hana haja ya kubaki na alama yoyote kwasababu inamkubushia machungu.

Alisema alijitahidi kuvumilia lakini anaona machungu yanaongezeka hivyo anahitaji kuifuta ili kuwa sawa.

“Nimepitia maumivu na machungu mengi hivyo sihitaji kubaki na alama ya mtu ambayo nimempoteza hivyo ninampango wa kuifuta ili kumsahau kabisa".

Itakumbukwa, Barnaba na Zuu walijaliwa kupata mtoto mmoja wa kiume na kumpa jina la #Steve. Mama Steve amefunga ndoa wikiendi iliyomalizika na mpenzi wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad