Birthday ya Mtoto wa Hamisa Yazua Jambo...Lulu Michael Agoma Katu Katu Kumpost Afunguka Haya


Siku ya Aprili 10, ilikuwa ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa mtoto wa staa wa filamu, muziki na video vixen Hamisa Mobetto aitwaye Baby Fansy ambaye alikuwa anatimiza miaka mitano.

Kupitia show ya "FNL" ya EATV  Hamisa Mobetto ameulizwa angejiskiaje kama mtoto wake angepostiwa na Elizabeth Michael "Lulu" ambaye ndiyo mpenzi wa mzazi mwenziye ambapo amejibu,  "Mwanangu leo anatimiza miaka mitano, hata Lulu angempost mwanangu ni sawa tu ningeona kitu cha kawaida japo sisi tunaichukulia tofauti kwenye mitandao ya kijamii”.

Kwa upande wa Lulu  baada ya kushambuliwa na mashabiki kwa kutom-post mtoto wa mpenzi wake ameandika ujumbe mzito kwenye mtandao wa instagram ambapo ameeleza kuwa

"Jana ndiyo  nimeelewa kiasi  gani watu  tumeruhusu mitandao ichukue  zile akili za kuzaliwa kabisa, labda nijaribu ku-share jambo kwa huu uelewa wangu mdogo nilio nao, kupost mtu mtandaoni haimaanishi upendo  kama wengi wetu tunavyochukulia, kupost ni jambo la ziada tu" ameandika 

"Kwa mfano unampost mtoto wa miaka mitano ambaye hata Instagram haijui  unafikiri ndiyo njia anayoweza kuhisi upendo wako, sisemi kwamba haitakiwi au tusifanye, unaweza kuamua kufanya au kutokufanya kwa sababu ni ziada tu" ameongeza

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad