Waziri mkuu wa Uingereza , Boris Johnson awapongeza madaktari kwa kufanya kile kilichohitajika kunusuru maisha yake alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuambukiwa virusi vya corona.
Boris amewapongeza madaktari kwa kile alichojata kuwa wamenusuru maisha yake baada ya kulazwa hospitali akiwa ameambukiwa virusi vya corona.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson ameruhusiwa kuondoka hospitali Jumapili baada ya vipimo kuonesha kuwa hana maambukizi na kuwa afya yake ni salama.
Baada ya kuruhusiwa kuondoka katika hospitali ya Mtakatifu Thomas mjini London, waziri mkuu huyo ataendelea na uchunguzi akiwa nyumbani kwake Chequers.
Boris hatorejea sasa hivi kutekeleza jukumu lake la waziri mkuu hadi atakapothibitishiwa na madaktari kuwa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake.
Waziri mkuu huyo wa Uingereza amesema kwamba taifa lake limepiga hatua katika juhudi za kupambana na virusi vya corona.
Video iliopeperushwa katika ukurasa wake wa Twitter imemuonesha Boris akiondoka hospitali ambapo alikuwa akipatiwa matibabu yaliochukuwa muda wa wiki moja.