Shonza Ampa Madam Ritta Siku 30 Amlipe Mshindi wa BSS 2019 – Video



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza ametoa mwezi mmoja kwa uongozi wa Kampuni ya Benchmark Production inayoendesha mashindano ya kusaka vipaji kwa wasanii wa muziki (Bongo Star Search-BSS) kumlipa mshindi wa kwanza wa mwaka 2019, Meshack Fukuta zawadi yake TZS 50 milioni.


Shonza ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwa lengo la kueleza umma jitihada ambazo serikali imefanya baada ya kupokea barua ya malalamiko ya kuto kulipwa kwa mshindi huyo kutoka kwa familia yao.

Fainali za 10 za mashindano ya hayo nchini Tanzania zilifanyika usiku wa kuamkia Jumatano Desemba 25, 2019 ambapo Meshack Fukuta kutoka mkoani Mbeya aliibuka mshindi baada ya kuwa ameshiriki mara tatu pasina kushinda.

Mbali na kiasi hicho cha fedha alichoahidiwa kama mshindi wa kwanza, alipewa ofa ya kusimamiwa muziki wake kwa mwaka mzima ambapo pia atakuwa na meneja.

VIDEO:

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kamata, Sukuma Ndani..!!
    Funga ofisi na sitisha Leseni.

    Hii si Awamu ya kuwaonea Wanyonge.
    Wanyonge tuna Mtetezi wetu Baba JPJM..

    HAWA MATAPELI NA WADANGANYIFU KWA NI
    SEGERE AU BUTIMBA...NA KAKA BISWALO
    ANA KAZI HAPO YA ZIADA TUMSHIRIKISHE.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ndiyo maana namuona ananunua Brazilian hair na Peruvian kumbe
      ni Magumashi na madili,

      Mdada, amebugi stepu alifikiri
      Dogo atanyamaza Ki Ulaghai.

      Ndio mana Salama Akaondoka. kumuogopa MUNGU, SIRI IMEFICHUKA

      Naomba wizara iwatafute washindi wa toka 2014-2018 muwahoji kama walipata haki zao zilizo ahidiwa
      La Sivyo sheria na wizara husika zichukue taratibu zinazostahili.

      Haki ya mtu ni haki yake ni lazima imfikie hata kama ilichelewa pindi ikibainika.

      Hongera mama Shonza kumbe ulisha istukia to 24Dec. Hongera Mwakyembe usipate kigugumizi hapa Hii ni Awamu yetu kuwalinda na kuwatetea . Ndg. Majali ana monitor closely kama kawaida yake.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad