Chidi Benz "Niliambiwa Sitakiwi Kuingalia Yanayoendelea Dunia"

 
MwanaHipHop maarufu hapa nchini Chidi Benz, amefunguka kusema watu wake hawamruhusu yeye kutumia mitandao ya kijamii kwa sababu, aliambiwa hatakiwi kuyaona yale yanayoendelea duniani.


Chidi Benz ameiambia EATV & EA Radio Digital, sababu ya kuambiwa hivyo ni kukazania zaidi kwenye masuala yake ya kazi kuliko yale yanayoendelea duniani kupitia mitandao ya kijamii.

"Ukitaka kusema kuhusu mimi hakikisha wewe umekamilika zaidi yangu, pia siwezi kubishana na mtu wa mitandaoni kama amenitukana, japo kuna muda huwa naangalia kwenye mitandao lakini watu wangu hawaniruhusu kufanya hivyo maana niliambiwa sitakiwi kuiangalia hii dunia na mambo yanayoendelea ninachotakiwa kufanya ni kazi tu" ameeleza Chidi Benz.

Pia Chidi Benz ameendela kusema kwa sasa hata simu zake hashiki yeye kuna mtu anaitwa Saidi ndiyo anazimiliki na hayupo kwenye mambo ya mitandao.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad