China: WHO imesema Hakuna Ushahidi Virusi vya Corona ni vya Maabara



Wizara ya mambo ya nje ya China imesema Shirika la Afya Duniani, WHO limesema hakuna ushahidi kwamba virusi vya corona ambavyo vimewaathiri zaidi ya watu milioni 2 duniani vilitengenezwa kwenye maabara.

 Msemaji wa wizara hiyo, Zhao Lijian ameyasema hayo leo wakati akijibu swali kuhusu shutuma kwamba virusi vya corona vilianzia kwenye maabara katika jimbo la Wuhan nchini China, ambako janga hilo lilizuka kwa mara ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2019.

 Zhao amewaambia waandishi habari mjini Beijing kwamba maafisa wa WHO wamesema mara kadhaa kwamba hakuna ushahidi unaoonyesha kuwa virusi vya corona vilitengenezwa kwenye maabara.

Rais wa Marekani, Donald Trump jana alisema kuwa serikali yake inajaribu kutathmini iwapo virusi vya corona vimetokea kwenye maabara ya Wuhan na Waziri wa Mambo ya Nje, Mike Pompeo amesema China inahitaji kujisafisha kuhusu kile wanachokijua.

Zhao hakuzungumzia moja kwa moja kauli ya Trump.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad