Corona: Kipigo na Kuua, Polisi Wanne




HATIMAYE serikali ya Kenya imeonekana kuchukua hatua dhidi ya mauaji na ukatili unaoripotiwa kuendelezwa na maafisa wa polisi wanapoidhinisha amri ya kutotoka nje ya saa moja usiku hadi saa kumi na moja asubuhi.

 
Idara ya usalama imetangaza kuwa polisi wanne wamesimamishwa kazi kusubiri uchunguzi. Haya yanajiri huku watu wawili zaidi wakiripotiwa kuuawa katika maeneo ya Kakamega na Kwale. Marcus Ocholla, kamanda wa polisi mkoani Bonde la Ufa amethibitisha kupokea ripoti kadhaa kuhusu maafisa wa polisi kuwajeruhi raia.

 
Katika muda wa wiki moja sasa, kumekuwa na ongezeko la matukio ya maafisa wa polisi kutumia nguvu kupita kiasi kukabiliana na Wakenya wanaopatikana nje baada ya kuanza kwa muda wa marufuku ya kutembea usiku.


Watu 10 wanauguza majeraha na wengine wamelazwa hospitali kufuatia ukatili wa polisi
mjini Busia, wengine wakiwa wamelazwa hospitalini baada ya polisi kuingia kwa nguvu katika boma moja walimokuwa wamejifungia baada ya masaa ya kutembea kuisha. 


Ocholla ameeleza kuwa tayari wamechukua hatua ya kuwasimamisha kazi maafisa wanne wa polisi, huku wakuu wawili wakipewa uhamisho.

Kesi iliyowasilishwa na chama cha mawakili nchini kenya (LSK) kupinga uhalali wa amri ya kutotembea usiku iliyotangazwa na serikali itasikilizwa Aprili 9, 2020,  Hata hivyo, katika uamuzi wa awali polisi wameagizwa kutotumia nguvu katika kuidhinisha amri hiyo ya kutotoka nje.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad