CORONA: Masikini Kwenye Makazi Duni Wanalazimika Kufanya Kazi


''Kuna uwezekano wa mimi kufa kwa njaa kuliko kwa virusi katika hatua hii,'' anasema Pantira Sutthi, muuza chakula anayeishi kwenye eneo la makazi duni ya Klong Toei nchini Thailand.

Nyumba ndogo zilizojengwa kwa mbao zilizochakaa na rangi zilizofubaa kwenye eneo hilo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 1.5.

Bi Sutthi ni mama anayemlea mtoto wake pekee na mjukuu bila usaidizi wowote.

Huishi kwa kuuza kuku wa kukaanga na nyama katika shule moja iliyo karibu. Lakini chanzo chake kikuu cha kipato kwa sasa kimetoweka kutokana na janga la corona, lililofanya shule kufungwa.

Mara akawa ametoka kwenye kupata kiasi cha dola 30 kwa siku na hatimaye sasa hapati chochote.

Ameathirika kwa kiasi kikubwa na virusi, kama ilivyo kwa watu wengine 20,000 wanaoita eneo hili la Klong Toei nyumbani kwao.

Kwa bi Sutthi, kuhifadhi chakula ndani kwa ajili ya familia yake ni changamoto kuliko kununua vitakasa mikono au barakoa. Anaweza kugharamia kimoja au kingine.

''Ni bahati kuwa hakuna hata mmoja kwenye jamii yetu aliyeathirika, hivyo sitaugua wala kufa kutokana na virusi. Lakini umasikini unatuua taratibu,'' alisema.''Nina matumaini tu kuwa hali itaimarika hii karibuni, na nina matumaini serikali yetu itatusaidia.''

Katika hali ya kutokuwepo kwa watoto na wateja wengine kununua chakula anachopika, Bi Sutthi hawezi kukidhi mahitaji yake.

''Ninataka kweli kwenda nje kuuza chakula na kupata pesa,'' anasema . ''Lakini sina pesa za kununua chakula changu mwenyewe- wapi nitaweza kupata fedha ya kununua kuku na nyama kwa ajili ya kuuza? ''

Anaishi kwa kupata msaada wa chakula kutoka kwa ofisi za misaada na kwenye masinagogi.

''Kila ninaposikia kuhusu watu kutoa chakula bure kwenye eneo hili, ninakwenda na kujaribu kuchukua chakula cha kutosha kwa ajili ya familia yangu yote. Ninaogopa virusi, lakini kwa rasilimali chache na fedha hii ni njia pekee ya kuishi,'' Bi Sutthi anasema.

Mbali na dawa za kulevya na wizi, hakuna uchaguzi wa kazi walionao watu wanaoishi katika maeneo duni. Kama ilivyo kwa wengine wengi, Bibi Thongrueng Thongphuen ana miaka 56 anayefanya kazi kama kibarua anahangaika kupata fedha za kujikimu hivi sasa.

Sambamba na mumewe huondoka kila siku kwenda kwenye mtaani karibu na makazi yao kwa ajili ya kutafuta kazi za kibarua. Anafahamu kuhusu ushauri wa serikali wa kutotoka nje, lakini anahisi ni muhimu kutoka ili aweze kujipatia kipato kwa ajili ya kuishi.

''Watu masikini kama sisi hawana namna ya kufanya. Ninajua serikali inamtaka kila mmoja kusalia nyumbani. lakini kama sitatoka nje kujipatia fedha, hakuna atakayeweza kuishi ,'' Bibi Thongphuen alieleza.

''Hakuna aliyetupa kibaarua, tuko hatarini kupata maambukizi ya virusi tunapokuwa nje na huenda tukavibeba kuvipeleka kwenye jamii yetu. Lakini tutafanya nini? Watoto wangu lazima wapate chakula na watu wanaonidai huja kuchukua pesa zao nilizokopa. Niko katika shinikizo kubwa. Wakati mwingine, sioni umuhimu wa kuishi,'' alisema.

Klong Toei ni eneo kubwa zaidi la makazi duni nchini Thailand. Takribani watu 20,000 wanaishi eneo hili- ingawa idadi kamili inaaminika kuwa juu zaidi, labda karibu 100,000.

Nyumba zimejengwa katika mazingira ya msongamano, hali ambayo ni rahisi kwa ugonjwa kusambaa.

Watu wengi katika makazi hayo wanafahamu kuhusu virusi vya Covid-19, lakini kwa rasilimali walizonazo, hakuna cha kufanya zaidi ya kusaidiana wenyewe.

''Watu wengi katika jamii hii ni watoto, wazee, na wagonjwa wasioweza kutembea. Iwapo itatokea hatari ya maambukizi kwa mtu mmoja tu, jamii yote itakuwa hatarini,'' mkazi mwingine, Sanitmueanwai anaeleza.

Bi Ladda Mangmeepol ana miaka 26 anaishi kwenye eneo la makazi duni. Anatengeneza barakoa na kuwapa watu bure.

''Mimi ni mmoja kati ya watu wenye bahati ambao wamekuwa wakizitunza familia zao. Lakini nimekuwa nikiwaona shangazi zangu, wajomba, na majirani wanavyohangaika kwenye hali hii.''

''Wote ni vibarua na hakuna kazi kwa ajili yao kwa sasa. Huu ni mwezi wa kwanza wa janga mjini Bangkok na watu tayari wanapata tabu. Siwezi kufikiri hali itakuwa vipi mwezi ujao.''

''Hali inaogopesha yalipo makazi yangu: kuna mtu mmoja aliye na maambukizi ya Covid-19,'' anaongeza bi Mangmeepol. ''Ninawasiwasi kuwa watu wengi kwenye jamii yote wataambukizwa na kupoteza maisha kutokana na virusi hivi.''

Wakati raia wa Thailand wakipambana na janga , maelfu katika makazi duni ya Klong Toei wako katika hatari kubwa.

Ingawa serikali imemtaka kila mmoja kutotoka nje , kiuhalisia watu hawa hawawezi kufuata sharti hili.

Idadi ya watu walioambukizwa inaendelea kuongezeka nchini Thailand, kama ilivyo idadi ya vifo.

Serikali imeiweka Klong Toei kwenye orodha ya maeneo yanayopaswa kubomolewa ndani ya miaka kumi ijayo, lakini tayari inaonekana jamii ya eneo hilo imesahauliwa.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ndiyo Maisha..!!

    Tushukuru kuwa Tanzania.
    Tushukuru kuwa na Raisi km JPJM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad