Rais wa Brazil Jair Bolsonaro amemfukuza kazi Waziri wa Afya nchini humo Luiz Henrique Mandetta kisa ni hatua za kufuatwa katika kupambana na janga la corona n chini humo.
Jair Bolsonaro akiwa na Luiz Mandetta mwanzoni mwa mwezi Machi
Viongozi hao wawili wamekuwa wakivutana kwa wiki kadhaa juu ya mikakati ya Brazil ya kupambana na maambukizi ya virusi vya corona.
Mandetta amekuwa akipendekeza hatua za tahadhari za kuwataka watu kutengana na kuepuka mikusanyiko, wakati Bolsonaro kwa upande wake amekuwa akidai kwamba ugonjwa wa COVID-19 hauna tofauti na mafua ya kawaida yaliyozoeleka na kutaka watu kuendelea na kazi.
Bolsonaro pia amesisitiza hatua za kuweka tahadhari hazina ulazima na kwamba zitaumiza uchumi wa nchi. Utafiti wa maoni ya raia uliofanywa mwezi huu na kampuni ya Datafolha umedhihirisha kwamba asilimia 77 ya raia wa Brazil wamesema itiko la Wizara ya Afya chini ya uongozi wa Mandetta la kukabiliana na COVID-19 lilikuwa ni zuri. Na asilimia 33 ya walioshiriki utafiti huo wamempongeza Bolsonaro.