Mbunge wa Arusha mjini (Chadema), Godbless Lema amesema shule ama vyuo kuendelea kufungwa wakati baa , klabu, hoteli, masoko, stendi bado zinaendelea kawaida sio jambo nzuri.
Lema amesema suala la neno mikutano isiyo rasmi ‘Hivi Corona virusi ina ogopa mikutano rasmi?,”
Lema amesema wanaogopa kuchukua hatua lakini watakuja kuchukua hatua muda umeshachelewa.
Kiongozi huyo aliandika ujumbe huo katika ukurasa wake wa twitter kuwa “Shule/ vyuo kuendelea kufungwa wakati baa, club, hotel, masoko, stendi bado zina endelea kawaida bado sio kazi nzuri. Halafu!! hili neno mikutano isiyo rasmi hivi Corona Virus ina ogopa mikutano isiyo rasmi? Tuna ogopa kuchukua hatua lakini tutakuja kuchukua hatua huku tukiwa tumechelewa sana,”.
Shule/Vyuo kuendelea kufungwa wkt baa,club,hotel,masoko,stendi bado zina endelea kawaida bado sio kazi nzuri.Halafu!!hili neno mikutano isiyo rasmi hivi Corona virus ina ogopa mikutano rasmi ?Tuna ogopa kuchukua hatua lakini tutakuja kuchukua hatua huku tukiwa tumechelewa sana— Godbless E.J. Lema (@godbless_lema) April 14, 2020